Download Mp3 from African

LEMBELI ATOA YA MOYONI MBELE YA RAIS MAGUFULI KWANINI ALIHAMA CCM

ALIYEKUWA Mbunge wa jimbo la kahama  James Lembeli amesema kuwa aliamua kujitoa katika Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutokana na chama hicho kukithiri katika rushwa, Ufisadi pamoja na unafiki.

Lembeli aliyasema hayo mbele Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia Wananchi wa Mji wa Kahama ikiwa ni pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kkukipa ushindi chama cha mapinduzi katika kuchaguzi Mkuu uliopita.

“Iwapo Mwenyekiti wa chama cha Mapionduzi  Taifa ambaye ni Rais John Pombe Magufuli  atakisafisha chama hicho basi namimi ninaseza kurudi katika chama hicho kwa lengo lakuwahudumia Wananchi”,Alisema James Lembeli aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama.

Alisema kuwa anashukuru Rais Magufuli kwa kuja katika Wilaya ya Kahama na kuongeza kuwa yeyer hana kinyongo na Wataendelea kusalimiana kwani kubadilisha msikiti sio mwisho wa uislamu.

Aidha aliendelea kusema kuwa kama Rais Magufuli akikisafisha chama hicho yeye hana budi kurudi kundini kwani kwa sasa bado anasubiri kiongozi huyo kukisafisha chama hicho kwa kuwa kimejaaa watu ambao hawana sifa ya kukiongoza chama hicho.

Hata hivyo Rais John Mgufuli alisema kuwa yote aliyoyahaidi atayafanyia kazi na kuongeza kuwa hatalewa madaraka ya Urais na kuwataka Watanzania kumtanguliza Mungu katika kazi wanazozifanya za kila siku.

“Wanakahama tambueni kuwa Lembeli ni Rafiki yangu wa siku nyingi na kuwepo kwake hapo ninategemea mabadiliko makubwa kutoka kwake na ninakushauri urudi Tanzania kwani ulikokwenda ulikuwa umepotea njia’’, Alisema Rais John Mgufuli.

Aidha Rais Mgufuli alimtaka James Lembeli kurudi katika Chama cha Mapinduzi kwani huko aliopkuwa ameamua kwenda ndiko kwa sasa walipo hao Mafisadi ambao alikuwa akiwazungumzia kila siku.



“Ninakuomba Lembeli urudi kundini mimi ninakujua unavyowapenda Wananchi wako wa Kahama na ukirudi sikta kukata mkia kwani huko ulikokwenda umepotea njia na mimi ndio mwenyekiti niyekuwa ninapigania Wanachama wasaliti ambao asubuhi wapo CCM jioni wapo Upinzani”, Alisema Rais John Mgufuli.




Tag : lainnya
Back To Top