Download Mp3 from African

MKUU WA MKOA WA SIMIYU ANTHONY MTAKA ASEMA OLE WAO WATAKAO ANDAMANA

Wakati Chama cha demokrasi na Maendeleo (Chadema) kikitangaza kuwa  kufanyika kwa maandamao nchi nzima kwa kile walichokiita kupinga matukio ya ukandamizaji wa haki za binadamu serikali Mkoani Simiyu ametoa onyo kali.

Wiki iliyopita chama hicho kupitia kwa Mwenyekiti wake Taifa Filimani Mbowe alitanga  kufanyika Maandamano na mikutano kwa wanachama na wafuasi wao kupinga hali hiyo.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu jana akiongea na mamia ya wananchi wa Mkoa huo katika viwanja vya mpira wa pete vilivyoko mjini Bariadi, aliwataka wale wote ambao wamejiandaa kwa ajili ya maandamano kusitisha mpango huo.

“ kwa nia njema bila ya hata kufikishana mbali na leo niwatangazie wale ambao mmejiandaa jumatatu (leo) kwenda kwenye maandamano, niwaombe sitisheni huo mpango kwa nia njema” Alisema

Mtaka ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usala alieleza kuwa “Ole wake mtu ajipange au kuandaa kwenda kwenye maandamo, sitakuwa na msamalia mtume, ukitaka kuona nguvu niliyonayo andamana jumatatu (leo)” Alisema

Aliwataka wanasiasa Mkoani humo pamoja na wafuasi wake kutumia siku hiyo katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa chini likiwemo suala la uchangiaji wa Madawati kwa shule za msingi na sekondari.

Aidha aliongeza kuwa agizo la Rais John Magufuli ni kuwa wanasiasa wale walioshinda nafasi za ubunge, udiwani kuwa wao wanaruhusiwa kufanya mikutano muda wowote katika maeneo yao wanayotawala.

“ juzi Rais ametoa maagizo, kama mmesikia natumaini hakuna mtu yeyote atakayekwenda au kuandaa maandamano, niwaombe wanasiasa tusaidiane katika kujenga nchi na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi” Alisema Mtaka.

.


Tag : lainnya
Back To Top