Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema na Ukawa, Edward Lowassa amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Mnauye leo katika jumuiko la kuuaga mwili wa aliyekuwa Mpigapicha wa Tanzania Daima, Joseph Senga.
Mwili wa Joseph Senga (58) umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwao, Shushi-Nyambichi, Kwimba mkoani Mwanza kwa ajili ya maziko hapo kesho.
Mwili wa Joseph Senga (58) umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwao, Shushi-Nyambichi, Kwimba mkoani Mwanza kwa ajili ya maziko hapo kesho.
Akizungumza wakati wa kuuga mwili wa marehemu Dar es Salaam mapema leo, msemaji wa familia, Charles Kapama amesema maziko yatafanyika kesho saa nane mchana baada ya mwili kuwasili kijijini.
Viongozi mbalimbali walijumuika na ndugu, jamaa na marafiki wa familia hiyo kuuga mwili wa marehemu Senga ambaye alifariki dunia Julai 27 katika hispitali ya BLK, New Dehli Republic of Republic of India alikokwenda kupatiwa matibabu, katika uwanja wa mpira uliojirani na nyumbani kwake, Sinza jijini hapa.
Tag :
lainnya