Habari hii imeripotiwa na BBC Swahili ambapo imesema kwamba Rais wa Nicaragua Daniel Ortega amemtaja mkewe kama mgombea mwenza na makamu wa rais wakati huu ambapo anawania kuchaguliwa kwa muhula mwingine.
Mkewe Rosario Murillo tayari ana wadhfa maarufu wa msemaji wa serikali na anaonekana kuwa anagawana mamlaka na mumewe. Wakosoaji wanawashtumu wanandoa hao wawili kwa kuiendesha Nicaragua ambayo inakabiliwa na uchaguzi mkuu mwezi Novemba kama chombo chao cha binafsi.
Rais Ortega ambaye si mzungumzaji sana katika vyombo vya habari, mkewe huonekana mara kwa mara katika runinga akijadili sera na kujikuza. Akiwa mama wa watoto seven wa rais huyo anajua kuongea Kiingereza na Kifaransa huku akijulikana pia kuwa mshairi.
Mume na mkewe waliwasilisha makaratasi yao ya kugombea viti hivyo rasmi katika mji mkuu wa Managua wakiandamana na mshauri ambaye ni wakili wa chama chao cha Sandinista.
Tag :
lainnya