Download Mp3 from African

Vanessa Mdee ajibu tuhuma za Timbulo kuwa alimpigia simu kutaka collabo akamwambia hamjui

Muimbaji wa ‘Ngomani’ Timbulo amesikika kwenye kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV akimtupia lawama Vanessa Mdee kuwa alimpigia simu kumuomba amshirikishe kwenye wimbo wake lakini akamweleza kuwa hamjui.
Timbulo
Amedai kuwa kitendo hicho kilimnyong’onyeza kwa kuona kuwa ni kama muimbaji huyo amemletea pozi ilhali ana uhakika kuwa atakuwa anamfamu.
Nimemtafuta Vanessa kumuuliza kuhusu malalamiko hayo ya Timbulo na alikuwa na haya ya kusema:
“Kusema kweli sikumaanisha kumdharau au kumwonesha kwamba simfahamu Timbulo bali siku zote mtu akiwa anakupigia na namba hauna kitu cha kwanza utauliza ‘haloo haloo, nani mwenzangu’ akasema Timbulo, nikasema ‘Timbulo nani?’ sikumaanisha kwa ubaya lakini kama amechukulia kwa ubaya naomba anisamehe na I promise everything is cool together with I want him all the best.”
Timbulo pia alimtupia lawama Malaika kuwa alimletea mapozi licha ya kumsaidia sana kipindi ambacho hajulikani.
Tag : lainnya
Back To Top