Download Mp3 from African

Wasanii Ude Ude na Iqu Junior wauawa katika tukio la ujambazi Tanga

Marehemu
Marehemu Ude Ude wa kushoto na rafiki yake Iku ambao wote wamefariki kwenye tukio hilo
Iqu Junior amewahi kumshirikisha Alikiba kwenye wimbo wake ‘Nisamehe.’
 Msanii na mtunzi wa nyimbo za Bongo Flava, Hamid Hafidh maarufu kama Ude Ude na rafiki yake Iku wameuawa katika tukio la ujambazi mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi wawili hao walikuwa miongoni mwa majambazi wanne waliokuwa na gari aina ya Toyota Probox waliokurupushwa na polisi katika jaribio la kuiba vifaa vya magari ya halmashauri.
Tukio hilo lilitokea jana saa mbili asubuhi walipokutwa wakivunja gari la mwalimu wa shule ya sekondari, Maweni aliyejulikana kwa jina la Commonwealth of Dominica Tarimo.
Wananchi wakiwa na piki piki na magari pia waliungana na polisi kuwafukuza watu hao na kuwashambulia. Polisi hao wamedai watu hao walijihami na silaha zenye ncha kali ili kujiokoa na wawili kupiga risasi huku wawili wakitokomea kwenye msitu ulio jirani na kiwanda cha saruji cha Sungura.Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga, Leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Tag : lainnya
Back To Top