Mané na Shasir |
Klabu kutoka nchini Rwanda Rayon Sport imemsajili mchezaji mrundi atakaye saidiana na mchezaji mwingine mrundi, Pierrot. Kwa mjibu wa Ruhagoyacu inasema kuwa klabu ya Rayon Sport imemsajili mchezaji mwingine mrundi, Nahimana Shasir ambaye amekuwa akiichezea klabu ya Vital'o pia na timu ya taifa ya Burundi, Intamba Murugamba.
Nahimana Shasir ni mchezaji wa soka mwenye wa miaka 23 na ana ndoto kubwa ya kuwa mchezaji bora, na ni mchezaji wa kati uku anakipaji ya hali ya juu. Namba kumi uyo wa Intamba Murugamba ndiye ameteuliwa mchezaji bora msimu uliyo malizika na amejiunga na Vital'o akitokea katika klabu ya Inter Star, na ameanza kuichezea timu ya taifa mwaka 2014, amecheza michuano ya CHAN 2014 nchini Afrika Kusini.
Tuwakumbushe kuwa Nahimana Shasir atamkuta mchezaji Kwizera Pierrot katika klabu ya Rayon Sport na pia ni mchezaji ambaye wanacheza wote katika timu ya taifa, Shasir ndiye mchezaji wa pili kusaini na Rayon Sport baada ya Ishimwe Issa Zapi akitokea Sunrise Fc.
Kila la kheri Nahimana Shasir, ..