Kampuni ya network ya Marekani, Yahoo imenunuliwa na kampuni ya mawasiliano ya Verizon Communications kwa dola bilioni 5, fedha taslimu.
Yahoo itaunganishwa na AOL, kampuni nyingine ya network iliyopoteza umaarufu ambayo nayo ilinunuliwa mwaka jana na kampuni hiyo. Hata hivyo dili hilo halijumuishi hisa za thamani ilizonazo kwenye kampuni ya China, Alibaba.
CEO wa Yahoo, Marissa Mayer
Fedha hizo ni ndogo zaidi kuliko dola bilioni 44 ambazo kampuni ya Microsoft ilitaka kuinunua Yahoo mwaka 2008. Yahoo iligoma kununuliwa kwa kiasi hicho cha fedha. Enzi za umaarufu wake, Yahoo ilikuwa na thamani ya dola bilioni 125.
CEO wa saba na wa mwisho wa Yahoo, Marissa Mayer, anadaiwa kuwa ataondoka baada ya dili hilo huku akilipwa kiinua mgongo cha dola milioni 50.

Tag :
lainnya