Meneja (Marketing Director) wa rapa Darassa wa Bongo Fleva, Lyeme Abdulfatah Ally aliwasili nchini Republic of Burundi kwakukamilisha ujio wa msanii wake na kutazama mazingira na mpangilio mzima wa demo inayosubiriwa na wapenzi wa muziki wa Burundifleva, Apr 08, 2017.
Meneja huyo alisema ameipenda Republic of Burundi na mazingira yoote uku akifurahia mapokezi na utulivu wa nchi akiamini kuwa msanii wake anazidi kuiteka Afrika na dunia nzima.
Lyeme Abdulfatah Ally aliwahidi wapenzi wa muziki kuwa chakufanya ni kufika kwa wingi siku ya demo kwa kushuhudia demo ya kibab-kubwa fikeni mapema kwajili watu watakua wengi kutoka nchi mbali mbali, njooni tucheze muziki tuache maneno ili tupate burundani tosha, alisema Meneja wa rapa Darassa.