Wasanii wanaounda Kundi la Scorpion Girl, Baby Madaha na Isabela pamoja na Kabula wamedai walishindwa kuachia kazi zao mpya za kundi kwa wakati kutokana na jina lao kufanana na jina la mtuhumiwa Scorpion mtoboa macho ambaye anakabiliwa na shtaka la kuhusika kwenye tukio la kupora na kumtoboa macho, Said Ally Mrisho.

Jumatatu hii mmoja kati ya wasanii hao, Isabela amedai kama wangeachia kazi mpya kipindi sekeseke hilo likiendelea huwenda wangefikiriwa vibaya na jamii.
“Kusema kweli kitu ambacho watu hawakijui Scorpion mtoboa macho ameharibu mipango yetu mingi sana sisi kama Scorpion Girls, ukiachana na kufanana kwa jina sisi na yule kaka lakini pia yele kaka tulikuwa tunaigiza naye kwa Mr Chuzi, sasa lilivyokuja kutokea hilo tukio kila mtu akawa anashangaa,” alisema Isabela.
Aliongeza, “Tukaona tukiachia projection mpya ya Scorpion Girl na huyu jamaa amepachikwa jina la Scorpion mtoboa macho, isingekuwa effect nzuri kwa sababu pia tulikuwa tufanya naye kazi, kwa hiyo huwenda ingetuletea matatizo makubwa sana,”
Kundi hilo wiki hii limeachia video mpya ya wimbo ‘Marioo’.

Tag :
lainnya