Download Mp3 from African

KIPIGO CHA 4-0 KUTOKA KWA EVERTON CHAANDIKA HISTORIA MPYA KWA GUARDIOLA ...asema ubingwa ndo basi tena


KOCHA wa Manchester City Pep Guardiola amekiri kuwa kipigo cha 4-0 kutoka kwa Everton kimekatisha matumaini yake ya kutwaa taji la Premier League.
 

Guardiola amebainisha kuwa pengo la pointi 10 kati ya City na Chelsea inayoongoza ligi ni mlima mrefu kuupanda. 
Aidha kocha huyo amesema hiki ni kipigo cha kwanza kikubwa kukipata kwenye mechi za nyumbani akiwa kama kocha. 
"Hii ni mara ya kwanza, sijawahi kupokea kipigo kizito namna hii, haijawahi kutokea hapo kabla na nitahitaji kujua ni kwanini," alisema Guardiola.
Tag : Michezo
Back To Top