Mutayarishaji pia muigizaji akiwa kiongozi wa Kampuni Tambwe The Great Filams ya uigizaji filamu nchini Burundi, Tambwe ametangaziwa kifo baada ya picha zikizagazwa kwenye mitandao za kijamii ikiwa na muonekano kama muigizaji huyo ameuawa.
Baada ya kutangaza filamu yake mpya ameandaa akiwashrikisha ma Staa kibao kama Jay Fire na mrembo Divine, habari nyingine imejitokeza kuhusu muigizaji Tambwe ambaye ni mmoja wa waigizaji wa kiume wachache wenye mashabiki wengi zaidi. Na katika hilo amefungua miradi mingi akitumia jina lake mfano ni hii Kampuni ya Tambwe The Great Filams.
Pamoja na watu kuona mambo yanamunyookea staa huyo, Tambwe ametangaziwa kifo na kuweka hofu kwa mashabiki zake , tumejaribu kumtafuta katika njia zote simu yake ya mkononi imezimwa nasi pia tukaamini habari hiyo.
Baada ya siku moja Staa huyo ameandika kwenye ukurasa wake wa facebuk kama ni mzima kiafya na kwamba picha zinazozagazwa ni picha za filamu yake mpya anayo iandaa na wa staa kibao.
habari za ukweli ni kwamba staa huyo wa Kampuni Tambwe The Great filams hajafa na siku chache mtashuhudia filamu mpya akishrikiana na ma staa wa Burndi Fleva.