CHAMA cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) kimesema kitasitisha huduma ya kusafirisha abiria kwenda mikoa yote nchini Jumapili ili kufanya ukaguzi wa mabasi yake, hatua ambayo itakuwa sawa na mgomo.
Aidha, Taboa imesema inapinga uamuzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) kutangaza kuyafungia mabasi yote ya kampuni ya City Boy badala ya moja ambalo lilisababisha ajali mkoani Singida hivi karibuni.
Julai 4, mabasi mawili ya kampuni hiyo yaligongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu zaidi ya thirty wilayani Manyoni mkoani Singida.
Taboa imesema pia itaipeleka serikali mahakamani kutokana na kufungiwa kwa mabasi hayo kwani kwa mujibu wa sheria, aliyetakiwa kulifungia ni waziri mwenye dhamana na si Sumatra kama ilivyofanyika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kumaliza kikao cha dharura cha wamiliki wa mabasi ya mikoani, Katibu wa Taboa, Enea Mrutu, alisema hawatakatisha tiketi kuanzia Jumapili ili kujipa muda wa kukagua mabasi yao kama yana uwezo wa kufanya safari ama la.
"Tumeamua kwa pamoja kuwa, kwa sababu tayari tumeshafanya 'booking' ya abiria, kuanzia Agosti 21 mwaka huu, tuanze kufanya ukaguzi wa mabasi yetu kote nchini ili yale ambayo hayana sifa yakae pembeni na yale yanayostahili kusafirisha abiria yafanye hivyo, kuliko utaratibu huu wa serikali wa kuyafungia yote bila kujali gari lililohusika kwenye ajali," alisema Mrutu.
Aidha alisema wanapinga vikali agizo la Sumatra la kuyafungia mabasi threescore ya kampuni 12 kwa makosa ya kusababisha ajali na wanataka mabasi yanayohusika pekee ndio yafungiwe.
Alizitaja kampuni zilizofungiwa mabasi yake kuwa ni Mohamed Trans, City Boy, Ota High Class, Kisbo Safari, Kisbo Express, Lubonelo na Kanda Safari.
Tag :
lainnya
