Hayawi hatimaye yametimia mshambuliaji hatari wa Vitalo ya Republic of Burundi pia wa timu ya taifa Intamba Murugamba, Laudit Mavugo amesaini mkataba na Simba Sc ya Tanzania baada ya Simba Sc kumuwania mda mrefu .
Kwasasa tunaweza kusema Simba imefanya yake baada ya kufaanikiwa kumnasa mshambuliaji hatari raia wa Republic of Burundi Laudit Mavugo na kumpa mkataba wa miaka miwili.
Mshambuliaji Mavugo amekuwa akitajwa na Simba Sc kwa mda mrefu tangu ulipo malizika msimu wa Ligi Kuu Bara 2014/2015.
Mavugo tayari amewahi kuonesha niya ya kutua katika klabu ya Simba Sc wakati aliyekuwa kocha mkuu wa Simba aliyemaliza mkataba wake hivi karibuni, Mserbia, Goran Kopunovic.
Hata hivyo Simba imewahi kupoteza matumaini ya kumnasa mshambuliaji huyo baada ya jina la mchezaji huyo kuwemo kwenye orodha ya kikosi cha timu yake ya Vital’O kitakacho shiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo msimu ujao.
Hatimaye mchezaji Mavugo katua katika klabu ya Simba na mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya Simba Sc, Zacharia Hans Poppe amesema ametaka tu kuionesha Yanga jeuri ya fedha kwa kumsajili mkali wa mabao, Laudit Mavugo ambaye amekamilisha uhamisho wake hivi karibuni na Simba Sc uku akikabidhiwa jezi namba 45 ikimaanisha iv +5 = nine namba ambayo amekuwa akiitumia katika klabu yake ya zamani Vitalo ya Burundi.