Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametii lile agizo la viongozi wote kuhamia mjini Dodoma huku akisema yeye atakuwa wa kwanza kuhamia huko.

Ameyasema hayo Jumatatu hii katika maadhimisho ya kuwakumbukua mashujaa waliolipigania taifa yaliyofanyika mjini humo. Amewaambia wakazi wa Dodoma kuwa mnamo mwezi wa tisa atakuwa tayari ameshahamia huko.
“Nimemuita waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu na katibu mkuu, nimewaambia wakamilishe nyumba yangu nahamia mwezi wa tisa haraka sana pale juu mara moja,” alisema.
“Kwahiyo mimi nikitangulia mwezi wa tisa mawaziri wote wanifuate. Moja tuhakikishe Dodoma ni kisiwa cha amani na pili watu wanakuja na tunaamini mamaziri, mabalozi wanaotoka nje watakuja Dodoma, tunahitaji huduma mbalimbali Dodoma, jipangeni sasa kuwekeza serikali hii ilivyosema tunatoa fursa hizi ndio fursa. Ongezeni hoteli za kitalii, ongezeni nyumba za kulala wageni, jengeni mahoteli makubwa, andaeni mazingira ya nyie kupata tija kufuatia ujio wa mawaziri mbalimbali na wageni kutoka nchi mbalimbali, huo ndo wito wangu,” alisisitiza.
Pia aliwashukuru wote walioudhuria maadhimisho hayo na kumshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kumpa nafasi ya kuongea na wananchi wa Dodoma na Watanzania kwa ujumla.

Tag :
lainnya