Tresor Ndikumana ni mchezaji wa klabu LLB Academic ya daraja ya kwanza kwenye Ligii Kuu Primus League nchini Burundi.
Baada ya kuangalia mechi kadhaa za Ligi Kuu msimu huu, African Mishe itawaletea kikosi bora cha msimu 2016/17 kitakachotokana na maoni ya mashabiki, makocha wengi wa Ligi hiyo na maoni ya wachezaji wengi wa ligii hiyo waliowapendekeza kutokana na ubora wao msimu huu.
Muandishi wetu aliweza kumfuatilia kiungo wa klabu ya LLB, Ndikumana Tresor na kutambua kuwa kati ya wachezaji wanaofanya vizuri kwenye klabu za Burundi, Tresor Ndikumana ni mmoja wao, baada ya kuaminiwa na kocha wake katika kikosi cha kwanza na katika timu ya taifa mwaka huu, sifa yake kubwa ni kupandisha mashambulizi ya timu na kurudi kukaba kwa haraka.
Tresor Ndikumana anazidi kuiunganisha timu yake kwa kukokota mpira vizuri, kupiga pasi nzuri na kufunga mabao anapopata nafasi.
Aidha, Tresor Ndikumana anazidi kuchangia kiasi kikubwa kuipelekea LLB kuchukua ubingwa msimu huu kama mambo yataendelea kuwa vizuri kwasababu timu yake inazidi kuwa kileleni kila wiki.